Hati za Kisheria

Pata maelezo ya kila unachohitaji kujua kuhusu mikataba yetu ya kisheria na sheria na masharti ya biashara.

Matangazo

Novemba 15, 2024

A. Exness (SC) Ltd sasa ni mtoa huduma za ODP aliyeidhinishwa na FSCA nchini Afrika Kusini

Sasisho Muhimu: Marekebisho ya Mkataba wa Mteja

Tuna furaha kutangaza kwamba Exness (SC) Ltd imeidhinishwa kama Mtoa Huduma za Bidhaa Moja kwa Moja (ODP) na Mamlaka ya Maadili ya Sekta ya Kifedha (FSCA) nchini Afrika Kusini.

Kama sehemu ya hatua hii muhimu, tumesasisha Mkataba wetu wa Mteja ili kujumuisha Kiambatisho A, ambacho kinaonyesha masharti ya ziada yanayosimamia uhusiano wetu wa kibiashara na wateja na washirika wetu walio nchini Afrika Kusini. Tafadhali kumbuka kuwa Kiambatisho A kinatumika kwa wateja wa Afrika Kusini pekee na hakiathiri wateja kutoka maeneo mengine.

Mkataba uliosasishwa wa Mteja, pamoja na Kiambatisho A, sasa unapatikana kwenye tovuti yetu. Tunahimiza wateja wote wa Afrika Kusini kuukagua kwa makini ili kuelewa sheria na masharti yanayotumika kwa huduma zetu. Zaidi ya hayo, tunapendekeza kwamba wateja wote, bila kujali mahali walipo, wakague Mkataba uliosasishwa wa Mteja kwa ujumla wake, kwa kuwa uendelezaji wa uhusiano wa kibiashara na Exness (SC) Ltd utachukuliwa kuwa unakubali masharti haya yaliyosasishwa.

Asante kwa imani yako kwa Exness (SC) Ltd.

B. Tangazo la Jumla:

Tungependa kuwajulisha wateja wote wa Exness (SC) Ltd, Exness (VG) Ltd na Exness B.V., kuwa hivi majuzi tulisasisha Mkataba wetu wa Mteja kama mojawapo ya juhudi tunazoendeleza za kuboresha utoaji wetu wa biashara na kuboresha vipengele muhimu vya uhusiano wetu na wateja wetu.

Tunakuomba ukague Mkataba wa Mteja uliosasishwa na ikiwa una maswali yoyote, tutumie barua pepe kwa support@exness.com. Timu yetu ya wataalamu wa Huduma kwa Wateja itakusaidia.

Fanya biashara na broker anayeaminika leo

Jionee mwenyewe kwa nini Exness ndiye broker anayefaa zaidi kwa traders zaidi ya 800,000 na washirika 64,000.