Biashara ya position: Kufuata mawimbi ya biashara ya stock ya muda mrefu
Stanislav Bernukhov
Mtaalamu Mkuu wa Kutrade wa Exness
Huu sio ushauri wa uwekezaji. Utendaji wa awali sio dalili ya matokeo yajayo. Mtaji wako uko hatarini, tafadhali fanya biashara kwa uangalifu.
Shiriki
Katika mwongozo huu:
- Mambo ya msingi ya biashara ya position
- Kuelewa mifumo ya kiufundi ya mikakati ya biashara ya position
- Udhibiti wa position ya biashara ya stock
- Jinsi traders wa position hudhibiti trade
- Kukokotoa mapato kwa kila stock
- Muhtasari wa biashara ya position kwa stocks
- Je, uko tayari kujaribu biashara ya stocks?
Biashara ya position, kwa ufafanuzi, ni mbinu ya kimkakati inayotumika katika masoko ya kifedha, hasa katika stocks, bidhaa, na ubadilishanaji wa fedha za kigeni (forex). Mbinu hii inahusisha kushikilia positions za biashara kwa muda mrefu: wiki, miezi, au hata miaka, kwa imani kwamba thamani ya mali itaongezeka katika kipindi hicho kirefu.
Inapotumika kwa soko la stock, biashara ya position inaweza kuwa muhimu sana, kwa kuwa stocks nyingi huwa na mabadiliko makubwa ya bei kwa muda mrefu.
Kwa mfano, stock ya TSLA ilikua kutoka $23 mwaka 2020 hadi kiwango cha juu zaidi cha $433 mwaka 2021*. Ingawa mwenendo ulikuwa ukibadilika-badilika, bado kulikuwa na fursa nyingi za muda mrefu za biashara kwa TSLA wakati huo.
Katika makala haya, tunaangazia mambo muhimu ambayo kila trader wa position anahitaji kukumbuka wakati wa kuunda mikakati ya biashara ya position kwa biashara ya stocks, ikiwa ni pamoja na uchanganuzi wa kiufundi na kimsingi, kutambua trends muhimu za muda mrefu, kuelewa mabadiliko ya soko na hisia za soko, na baadhi ya hatari zake ikilinganishwa na mikakati mingine ya biashara.
Mambo ya msingi ya biashara ya position
Kihistoria, biashara ya position imekuwa mtindo maarufu zaidi wa biashara katika masoko ya stocks baada ya uwekezaji wa kununua na kushikilia positions kwa muda mrefu, kwa kuwa masoko ya stock yanajulikana kwa mwelekeo wa muda mrefu wa kupanda kwa bei. Hii ni kweli hasa kwa masoko ya stock ya Marekani.
Je, kwa nini traders wa position wanapenda kutrade stocks?
Baadhi ya stocks zinazokua kwa haraka zinaweza kutoa mapato ya kila mwaka ya tarakimu mbili au hata tatu, ambayo yanalingana na trends zinazoendelea za muda mrefu. Hiyo ndiyo sababu biashara ya positions huvutia hasa kwa biashara ya stocks.
Sababu nyingine ambayo biashara ya stocks ya muda mrefu imekuwa maarufu ni kwa sababu kikao cha kawaida cha biashara kwenye soko la stock la NYSE au Nasdaq kina kikomo cha saa 6.5 kwa siku (kuanzia 09:30 hadi 16:00), ambayo inaweza kuchukuliwa kuwa dirisha finyu sana kwa biashara ya siku moja. Kutrade zaidi ya muda uliotajwa huchukuliwa kuwa “kabla ya soko kufunguliwa” au “baada ya soko kufungwa”. Viwango nje ya saa za kawaida za biashara hukuwa chini sana, kwa hivyo traders kwa kawaida hawafanyi biashara sana wakati huo.
Kufanya biashara ya siku moja kwa stocks kumezuiliwa kwa kipindi kidogo sana cha saa chache kwa siku. Kwa hivyo, biashara ya muda mfupi hadi ya kiwango cha kati na biashara ya positions ni mitindo inayofaa zaidi ya biashara ya stocks.
Biashara ya positions ikilinganishwa na biashara ya muda mfupi hadi muda wa kati kwa stocks
Biashara ya muda mfupi hadi muda wa kati na biashara ya position zinahusisha kushikilia trades usiku kucha (na wakati mwingine, wikendi). Hata hivyo, mitindo hii miwili ya biashara ina tofauti kadhaa, ambayo ni muhimu kuangazia.
Traders wa muda mfupi hadi wa kati wanalenga kunufaika kutokana na mienedo ya bei ya muda mfupi, na wanaweza kutrade katika pande zote mbili katika safu ya biashara ya muda mfupi. Kwa upande mwingine, traders wengi wa position wanahitaji trend ambayo inaendelea kwa muda ili kupata faida kubwa.
Ndiyo sababu, traders wa position wanahitaji kuzingatia uchanganuzi wa kiufundi na uchanganuzi wa kimsingi. Njia hii hukusaidia kutambua uwezekano wa “stocks zenye mienendo mikubwa” - stocks za kampuni ambazo zina uwezo wa ukuaji wa muda mrefu kwa upande mmoja, na thamani yake isikuwe juu sana, kwa upande mwingine.
Kuelewa mifumo ya kiufundi ya mikakati ya biashara ya position
Ikiwa wewe ni trader anayelenga kujiunga na mwenendo wa bei wa muda mrefu (trend ya muda mrefu), labda ungependa kujiunga mapema iwezekanavyo. Ndiyo maana mfumo maarufu zaidi wa biashara ya position ni breakout ya ‘kipindi kirefu bila mabadiliko ya bei’, kimsingi safu ya biashara ya muda mrefu.
Ingawa breakouts zinaweza kutokea kwa timeframes nyingi, zina umuhimu mahususi kwa traders wa position.
Mfano wa kwanza
Kwa mfano, TSLA ilipata breakout kubwa ya aina mbalimbali za biashara mnamo Septemba 2021. Kabla ya kupanda na kusogea juu zaidi, bei ilikuwa katika masafa mapana sana kati ya Aprili na Oktoba. Ilichukua miezi sita kukamilisha mfumo huo. Baada ya breakout, bei ya TSLA ilipanda kwa zaidi ya 50% hadi kiwango kipya cha juu zaidi.
Hapa tunaona chati ya stock ya TSLA mnamo Oktoba 2021 na breakout (yenye mduara) ya safu kubwa ya biashara. Chanzo: Tradingview.com
Mfano wa pili
Eli Lilly (LLY), kampuni ya dawa ya Marekani, ni mfano mwingine wa ‘mfumo wa kipindi kirefu bila mabadiliko ya bei.’ Ikiendeshwa na misingi thabiti, ilianzisha safu pana za biashara mara kwa mara. Safu ya tatu ilikiukwa kwa kiasi kikubwa mnamo Mei 2023, baada ya hapo bei ya LLY iliongezeka kwa zaidi ya 60%.
Katika soko la stock, matukio kwa kawaida huelekeza kwenye trends za soko za breakout ya kupanda kwa bei. Hata hivyo, stocks zingine zinaweza kuunda msingi na kuanza kushuka. Bei ya stocks pia inaweza kushuka, lakini trends za soko lenye bei inashuka kwa kawaida hufanya kazi kwa njia tofauti.
Mifumo ya kupanda kwa bei huchukua muda mrefu kuundwa, kukupa wewe, trader, muda mwingi wa kujiandaa. Kwa masoko ya kushuka kwa bei, mifumo huundwa haraka.
Unapofanya maamuzi ya biashara au kupanga mkakati wako wa biashara, sharti ufikirie soko la biashara ni kama kupanda ngazi, hatua moja kwa wakati. Kinyume chake, soko lenye bei inashuka ni kama kushuka haraka kwa kutumia lifti. Kwa ujumla, masoko ambayo bei inashuka ni bora kwa traders wa muda ffupi au wa kati au wa siku moja, lakini baadhi ya stocks bado hutoa fursa za kuingia kwenye trend ya muda mrefu ya kushuka kwa bei.
Chati ya stock ya LLY inayoonyesha breakout kubwa ya mfumo wa msingi mnamo Mei 2023. Chanzo: Tradingview.com
Mifumo ya kushuka kwa bei kwa kawaida huhusisha mifumo ya kawaida ya chati ya mabadiliko ya bei, kama vile vilele vitatu huku cha kati kikiwa juu kushinda vingine na vilele viwili.
Mfano wa tatu
Mfumo wa kawaida wa bei kwa biashara ya position unaweza kuonekana katika stock ya Intel (INTC). Iliunda muundo mkubwa wa vilele vitatu huku cha kati kikiwa juu kushinda vingine ambao ulianza mnamo Juni 2022. Mwenendo huu wa bei uliendelea hadi Oktoba 2022, na kusababisha bei kushuka kwa takriban miezi minne. Stock hiyo ilipoteza zaidi ya 40% ya thamani yake katika kipindi hiki kirefu. Kwenu traders, kudumisha position ya uuzaji kunaweza kuwa fursa nzuri, haswa ikiwa imeunganishwa na trade ingine ya ununuzi.
Chati ya stock ya INTC: muundo mkubwa wa vilele vitatu huku cha kati kikiwa juu kushinda vingine ulianzia mnamo Juni 2022. Chanzo: Tradingview.com
Udhibiti wa position ya biashara ya stock
Sharti uwe na subira huku ukingoja fursa sahihi. Hata hivyo, ni muhimu vile vile kudhibiti position yako ipasavyo mara tu unapoifungua, vinginevyo inaweza kuishia kufungwa haraka sana.
Zana kuu ambazo traders hutegemea kwa mikakati ya biashara ya udhibiti wa position ni orders za stop losses na trailing stop.
Kuweka order yako ya stop loss kama trader wa position
Sehemu ya mkakati mzuri wa biashara ya position ni kutambua kwa usahihi points za kuingia na kutoka na kutumia zana za kudhibiti hatari ili kuepuka kupoteza pesa haraka iwapo soko na mabadiliko ya bei yatatokea ghafla. Kwa hivyo, sehemu muhimu ya mpango wako wa biashara ya position ni kutumia zana ya stop loss katika timeframes zako zote za biashara. Hata hivyo, utahitaji kuweka stop loss yako kwa kiwango cha bei cha juu zaidi, kumaanisha kwa umbali mkubwa kutoka kwa bei ya kuingia ya position yako. Hii huzuia position yako kufungwa kwa sababu ya stop loss.
Miaka mingi iliyopita, wale wanaoitwa ‘Traders wanaoamini kuwa biashara inaweza kufundishwa na kwamba mikakati ya mafanikio ya biashara inaweza kutekelezwa kwa utaratibu’ walianzisha mpango wa biashara wa moja kwa moja wa kuweka stop loss. Wakiongozwa na Richard Dennis, mdadisi mashuhuri wa bidhaa anayejulikana kama "Prince of the Pits", traders hawa wa position walipendekeza kuweka stop loss mara mbili ya thamani ya Average True Range kwa timeframe ya kila siku.
Hebu tuchukulie kuwa ulifungua position ya uuzaji ya INTC mnamo Juni 2022.
Point ya kuingia kwa position ya uuzaji ilikuwa $43. Thamani ya ATR (20) kwa chati ya kila siku ilikuwa $1.57. Ungeweka stop loss kwa $3.14 kutoka kwa bei ya kuingia, ambayo ingekuwa $46.14.
Katika picha iliyo hapo juu tuna chati ya kila siku ya stock ya INTC kuanzia Juni 2022. Stop loss iliwekwa kwa mara mbili ya thamani ya indicator ya ATR katika $46.14. Chanzo: Tradingview.com
Je, ni nini kilitokea baadaye?
Tunaona kwamba baada ya kupungua kwa awali, bei ilipanda hadi $45, ikijaribu kurejea kwenye kiwango cha kuingia. Stop loss katika $46.14 ilikuwa salama na ililinda trade hii dhidi ya kufungwa mapema.
Chati ya kila siku ya stock ya INTC, Juni 2022. Stop loss, iliyowekwa katika $46.14, ilistahimili kurejea kwa bei ya kufunguliwa na ililinda position hii ili isifungwe mapema sana. Chanzo: Tradingview.com
Jinsi traders wa position hudhibiti trade
Traders wa position wanaweza kugundua kuwa mchakato hutofautiana wakati wa kuingia kwa trade.
Mienendo ya soko sio ya haraka kila wakati au inaypsonga katika mwelekeo mmoja. Badala yake, mabadiliko ya soko hutokea bei ikipanda na kushuka. Kanuni kuu hapa ni kungoja hadi kilele cha kupanda kwa bei kitakapofikiwa kabla ya kurekebisha stop loss yako juu ya kilele hiki, na kuweka stop-loss yako kwa umbali sawa na mara mbili ya thamani ya ATR.
Hebu tuchukue mfano kutoka kwa biashara ile ile ya INTC tuliyoonyesha hapo awali. Kilele cha kwanza cha kupanda kwa bei kilianzishwa kwa $38.82. Ungelazimika kuweka order yako ya trailing stop katika $41.99 (mara mbili ya thamani ya ATR, ambayo ilikuwa $1.36 wakati huo). Ingawa bei ilikuwa imeanzisha kilele kingine cha kupanda kwa bei juu ya kilele cha kwanza, stop loss haikubadilishwa tena.
Chati ya kila siku ya stock ya INTC, Julai 2022, inaonyesha kuwa order ya trailing stop ilistahimili mwenendo wa kupanda na kulinda position hiyo dhidi ya kufungwa mapema. Chanzo: Tradingview.com
Hatimaye, trade hii ingeweza kufungwa karibu na $28.85 na faida inayoweza kupatikana ya $14 kwa kila stock na hatari ya awali ya $3.14 kwa kila hisa, ambayo hutupatia karibu uwiano wa faida/hasara wa 5/1.
Chati ya kila siku ya stock ya INTC, Oktoba 2022. Position hiyo ilifungwa kwa order ya trailing stop loss. Chanzo: Tradingview.com
Uchanganuzi wa kimsingi wa biashara ya stock
Kuna mambo mengi ya kuzingatia unapofanya biashara ya stocks, lakini kipimo kimoja muhimu unachopaswa kuzingatia ni mapato kwa kila stock (EPS). Kipimo hiki huonyesha uwezo wa kampuni kupata pesa kwa wakati na kuongeza mapato yake.
Mapato kwa kila stock (EPS) ni kipimo msingi cha kifedha ambacho hutoa maarifa muhimu kuhusu faida na utendaji wa kifedha wa kampuni. Ni kiashiria muhimu kwa wawekezaji na wachanganuzi wakati wa kutathmini mvuto wa stock fulani.
Kukokotoa mapato kwa kila stock
Unaweza kukokotoa EPS kwa kugawanya mapato halisi ya kampuni kwa jumla ya idadi ya hisa zake zinazomilikiwa na wanahisa. Formula ni:
EPS = (Mapato halisi / Idadi ya Hisa Zake Zinazomilikiwa na Wanahisa)
Kimsingi, ikiwa kampuni inaonyesha mara kwa mara faida inayoongezeka robo baada ya robo, stock yake kwa kawaida huenda kwenye orodha ya ununuzi wa hedge funds na kusababisha ongezeko la mahitaji ya stock hiyo.
Kwa mfano, ukiangalia ubashiri wa robo mwaka wa EPS wa stocks za TSLA, utaona ubashiri wa ukuaji wa kudumu kwa robo zijazo.
Hii haimaanishi kuwa unapaswa kununua, lakini ni kiashirio chanya ambacho huongeza uwezekano wa breakouts za mwenendo wa juu.
Mienendo ya EPS ya robo kwa robo ya stock ya TSLA mnamo Oktoba 2023, ikiwa ni pamoja na mwongozo kwa robo zinazofuata. Chanzo: nasdaq.como
Muhtasari wa biashara ya position kwa stocks
- Traders wa position wanaweza kusubiri kutobadilika kwa bei kwa muda mrefu kuishe ili kuingia mapema katika biashara ambayo inaweza kudumu kwa miezi kadhaa.
- Udhibiti wa position ni muhimu kwa kuwa ni nadra sana kwa masoko kukua au kushuka katika mstari ulionyooka. Bei za mali kwa kawaida huunda awamu ya kawaida ya kupanda na kushuka.
- Traders wa position huunga mkono maoni yao ya kiufundi kwa kutumia vipimo vya kimsingi kama vile EPS au vipimo sawia, ili kuboresha uwezekano wa kufaulu.
Maswali yanayoulizwa sana
Je, ni stock gani bora kwa biashara ya position?
Stock bora kwa mkakati wa biashara ya position ni stock ya faida, ambayo daima hutoa mapato thabiti na faida, na ina misingi mizuri na mapato mazuri yasiyotarajiwa. Kwa kuongezea, ni bora kuchagua stocks za kampuni inayofanya kazi katika tasnia inayoongoza, kama vile teknolojia. Mfano mkuu unaweza kuwa AAPL (kampuni ya Apple), stock inayoongoza kwa teknolojia, inayojulikana kwa mwenendo wake wa juu wa muda mrefu na mtaji wake mkubwa wa soko. Kando na sifa hizi za kimsingi, stock inapaswa kuonyesha uchanganuzi thabiti wa kiufundi wakati wa kutumia indicators za kiufundi.
Je, biashara ya position ni bora kuliko biashara ya siku moja?
Mitindo ya biashara si mizuri au mibaya, lakini inahitaji kuendana na utu wako. Mpango wa biashara ya position sio wa kila mtu, kwa kuwa kudumisha positions za ununuzi kunamaanisha kuwa unaweza usipate faida yoyote kwa muda mrefu ikiwa hakuna trends za soko zilizopo. Biashara ya siku moja, kwa upande mwingine, hufuata utendaji wa muda mfupi. Tofauti muhimu ni kwamba ni changamoto zaidi kutokana na ushindani mkubwa wa kila siku na uwezo mdogo wa faida. Zaidi ya hayo, traders wa siku, moja huwa na uwezekano mkubwa wa kufanya makosa, kwa kuwa huwa wanafanya kazi kutokana na shinikizo la kihisia katika mazingira ya biashara ya kasi.
Kama trader wa position, unaweza kushikilia trade kwa muda mrefu na kuruhusu soko lifanye kazi, ikiwa umechagua stock sahihi na kutumia udhibiti ufaao wa hatari. Changamoto yako kuu ni kupata stock na muda sahihi wa kuingia.
Je, ni timeframe gani bora kwa traders wa position?
Kama trader wa position kwa kawaida ungetumia chati za kila siku. Hata hivyo, kila trader hutumia muunganisho wake wa kipekee wa timeframes ili kuboresha point yake ya kuingilia. Kwa mfano, unaweza kuchanganua chati ya kila siku na kuweka position kwa chati ya saa nne au ya saa moja. Licha ya hili, timeframe kuu ya trader wa position hubaki kuwa chati ya kila siku.
Je, ni mkakati gani wa biashara ulio bora kwa biashara ya position?
Tunapozungumza kuhusu biashara ya position, tunarejelea biashara ya muda mrefu inayofuata trend.Kama traders wa position wangependa kufuata trend ya muda mrefu, wanahitaji kutafuta iliyo thabiti kwanza, ambayo ina maanisha ya kuchagua stock thabiti na uwezo mzuri wa ukuaji na mising thabiti.
Traders wanahitaji kupata stock zinazofaa na wakati sahihi wa kuingia. Kwa kawaida, traders wa position hutafuta safu za biashara zilizopanuliwa ambazo zinakaribia kupata mienendo hivi karibuni. Breakout inapotokea, unaweza kujiunga na trend ya muda mrefu mapema kiasi, na hivyo kusababisha uwiano mzuri wa faida/hasara.
Je, ni aina gani ya akaunti ya Exness trade ninayopaswa kutumia kwa biashara ya stocks?
Kwa kweli, itakuwa bora kutumia akaunti ya kutrade yenye hali ya swap-free wakati wa kufanya biashara ya position, hata kama itagharimu zaidi. Swaps zinaweza kutumia sehemu ya faida yako ya biashara, lakini kwa kawaida sio kiasi kikubwa. Ikiwa unashikilia position kwa chini ya wiki moja au mbili, basi akaunti yoyote ya kutrade itaendana na mtindo huu wa biashara.
Je, uko tayari kujaribu biashara ya stocks?
Biashara ya position katika soko la stock inaweza kuwa mkakati mzuri wa uwekezaji wa muda mrefu , hasa wakati kuna mabadiliko makubwa ya bei kwa wakati. Kama tulivyojadili, ukuaji mkubwa wa TSLA katika miaka ya hivi karibuni ulitoa fursa nzuri kwa traders wa position. Ukiwa na maarifa na mikakati ifaayo, utakuwa na vifaa vyema zaidi vya kunufaika kutokana na trends hizi za soko la kifedha.
Kuchagua broker sahihi
Hata hivyo, kila safari ya uwekezaji ni ya kipekee na kuwa na mshirika anayeaminika ni muhimu. Hapa ndipo Exness inaweza kusaidia. Kwa utaalamu uliothibitishwa, tunatoa mifumo na zana thabiti, pamoja na masharti bora ya biashara kuliko ya soko, pamoja na hatua za ulinzi ili kuunga mkono juhudi zako za biashara. Hivyo kwa nini unasubiri? Anza kutrade katika Exness leo na ufurahie mabadiliko ya masoko ya kifedha.
Shiriki
Anza kutrade
Huu sio ushauri wa uwekezaji. Utendaji wa awali sio dalili ya matokeo yajayo. Mtaji wako uko hatarini, tafadhali fanya biashara kwa uangalifu.