Uwajibikaji wa Kijamiii
Sehemu ya kuwa kampuni yenye maadili ni kusaidia wengine na kufanya ulimwengu kuwa bora.
Maeneo tunayozingatia
Kuwa na maadili na kujali kumekita mizizi katika maadili na itikadi za Exness, pia kupata "Exness Way" yetu wenyewe. Katika Wajibu wa Shirika kwa Jamii tunalenga kuunda mbinu yetu wenyewe, na kuileta ili izingatie sehemu tofauti tunapoendelea.
Elimu
Elimu ndiyo msingi wa mabadiliko ya muda mrefu. Ndiyo maana tunawekeza katika miradi katika nyanja mbalimbali za elimu, iwe ni kwa kutoa vifaa muhimu kwa shule za msingi au programu bora za ufadhili wa masomo.
Mazingira
Ulinzi wa mazingira haujawahi kuwa muhimu zaidi. Tungependa kusaidia kwa upande wetu. Miongoni mwa programu zingine, tumeanzisha miradi ya upandaji wa miti ambayo tutapanua katika miaka ijayo. Pia tunaangalia hatua zetu za kimazingira, na kushirikiana na NGO za wataalam ili kuhakikisha uendelevu wa muda mrefu.
Dharura
Kwa kuwa kampuni ya kibinafsi yenye ufikiaji wa kimataifa, tunaweza kuleta athari ya kweli na yenye ufanisi wakati wa migogoro ya ndani na ya kimataifa. Tumetoa michango mikubwa katika kupambana na janga la Covid-19, na pia mioto ya misitu huko Cyprus. Pia tunahusika katika juhudi za kibinadamu zinazohusiana na shughuli za misaada wakati wa majanga kote duniani.
This is IT
Tazama wafanyakazi wa Exness wakihamasisha kizazi kijacho cha wataalamu wa teknolojia.
Cheza videoAhadi yetu kwa athari za kijamii
Tulizindua rasmi mpango wetu wa Exness CSR mnamo 2020 kwa kutoa michango kwa programu za usaidizi za COVID-19. Tangu wakati huo tumekuwa na bidii katika lengo letu la kushughulikia mahitaji ya jamii tunakofanya kazi.
Tangu kuanza kwa juhudi zetu, tulianzisha mipango kadhaa katika nchi nyingi kusaidia mazingira na jumuiya za eneo hilo. Wafanyakazi wa kujitolea wa Exness walishiriki katika mipango ya mazingira kama vile kusafisha ufuo na chini ya bahari, na kukusanya zaidi ya tani 1.5 za taka na kupanda zaidi ya miti 700.
Nchini Malesia, Wafanyakazi wa Exness walijitolea katika makazi ya mbwa walemavu, nchini Kupro baiskeli za mazoezi zilitolewa kwa shule ya watoto wenye ulemavu na kwa watu wenye ugonjwa wa Multiple Sclerosis. Nchini Kupro na Malesia, kompyuta na iPad zilitolewa kwa watoto wenye ulemavu wa kuona, na wafanyakazi wa Exness walishiriki katika hafla za uchangiaji wa damu. Nchini Vietnam tulifadhili mradi wa ujenzi wa daraja, na nchini Malesia kikundi cha wafanyakazi wa Exness kilisafiri msitu wa Malesia ili kukimu mahitaji ya kielimu ya, na kutoa usaidizi kwa, jumuiya ya wazawa wa Orang Asli.
kutoa
ufadhili 53 wa masomo katika nchi 5
kutoa
magari 4 ya kuzima moto kwa idara ya zima moto ya Kupro
kutolewa
kwa droni 3 kwa ajili ya kutambua na kuzuia moto
kutoa
€ milioni 1.1 kwa usaidizi wa matibabu wa COVID-19 na Exness
kuanzishwa
kwa zaidi ya mipango 30 ya Wajibu wa Kijamii wa Shirika la Exness
kutolewa
kwa mbao 350 za darasani kwa shule nchini Ushelisheli
nchi
10 kote ulimwenguni zimenufaika kutokana na mipango yetu ya CSR
kutolewa
kwa lita 14,000 za maji ya kunywa kupitia kituo chetu cha maji bila malipo
Kufanya biashara kuna jukumu na fursa ya kuleta matokeo chanya ulimwenguni. Tunafurahia kusaidia wengine.”
Petr Valov Afisa Mkuu Mtendaji
Boresha jinsi unafanya biashara
Jionee mwenyewe kwa nini Exness ndiye broker anayefaa zaidi kwa traders zaidi ya 800,000 na washirika 64,000.