Fanya trade kwa milisekunde
Upe mkakati wako manufaa unayostahili kwa utekelezaji wa haraka na wa kutegemewa, bila kujali ukubwa wa trade yako.
Je, kwa nini mchakato wa order execution ni muhimu
Iwe ni instant au market execution, kila pip ni muhimu kwa trader. Pip moja tu inaweza kumaanisha faida kubwa au hatari iliyopunguzwa. Ndio maana tunachukua jukumu letu la kutoa order execution ya haraka kwa umakini. Kadiri mchakato wa order execution ulivyo na ufanisi zaidi, ndivyo mkakati wako utakavyofanya vyema.
Order execution nzuri ndio jambo la msingi kwa mkakati wa biashara. Ni jukumu letu kama broker mkuu kuwa msingi huo kwa traders wetu.
Petr Valov
Mwanzilishi na Afisa Mtendaji Mkuu
Chagua aina ya execution unayopendelea
Exness inatoa aina mbili za order execution, zote zikiwa zimeundwa kwenye algoriti za kiwango cha juu ili kukupa uzoefu usio na hitilafu.
Instant execution
Hufungua trades kwa bei unayoomba au kuidhinisha, au haizifungui kamwe. Hii ni muhimu kwa traders ambao mikakati yao inahusu uhakika wa bei na ambao wana vigezo vikali vya udhibiti wa hatari.
Instant execution katika Exness
Algoriti zetu changamano zimeundwa ili kutoa bei thabiti ili uweze kufurahia mchakato rahisi wa execution kwa kiwango cha chini zaidi kinachowezekana cha requote.
Market execution
Hufungua trades kwa bei ya sasa ya soko inayopatikana. Hii ni muhimu kwa traders wanaofanya biashara sana ambao wanapendelea kuchukua fursa zinapotokea kwenye soko.
Market execution katika Exness
Miundombinu yetu, inayojumuisha mtandao wa kimataifa wa seva zilizogatuliwa huhakikisha ucheleweshwaji uliopunguzwa na slippage ndogo au isiyokuwepo kwenye market na pending orders, ili uweze kuboresha matokeo ya mkakati wako.
Mchakato wa order execution katika Exness
Hii ndiyo sababu zaidi ya traders milioni 1 wanaoendeleza biashara huchagua kutekeleza mikakati yao ya biashara katika Exness.
Fanya trade haraka kadri unavyoweza kubofya
Fungua, funga na ubadilishe orders katika milisekunde katika market execution inayotegemewa.
Furahia uwazi kamili
Jaribu mkakati wako kwa kutumia historia yetu ya tiki inayopatikana kwa umma au ukague utendaji wa mkakati wako ukilinganisha na bei zetu.
Tekeleza kwa bei ambayo ungependa
Nasa kila pip inayowezekana, kwa slippage ya market execution iliyopunguzwa na requotes za chini kwenye instant execution.
Jinsi inavyofanya kazi kwenye Terminali ya Exness
Furahia order execution ya ufanisi na rahisi kwenye jukwaa letu la biashara la Exness.
Fomu ya order inayofaa mtumiaji
Fungua orders kwa kutumia lot, sarafu au kiwango ukiwa na uchanganuzi wa kina wa ada, leverage, margin na zaidi kwa kila order.
Kufunga kundi la order
Badilisha au funga orders zako katika vikundi ili kuokoa sekunde na pips muhimu.
Biashara ya mbofyo mmoja
Wezesha hali ya biashara ya mbofyo mmoja kwenye Terminali ya Exness ili kuchukua fursa kwa haraka kupitia market execution.
Maswali yanayoulizwa sana
Je, order ya execution ni nini?
Order ya execution ni maagizo ya kununua au kuuza amana kwa niaba ya mteja. Broker anaweza kutekeleza orders hizi kwa kutumia njia mbalimbali, akilenga kufikia execution bora zaidi kulingana na masharti ya mteja'. Brokers wanahitajika kisheria kuhakikisha transactions zenye ufanisi kwa bei nzuri zaidi za soko. Katika Exness, orders hutolewa kupitia majukwaa ya biashara ya kidijitali kama vile Terminali ya Exness, Programu ya Exness Trade na MetaTrader 5. Kisha orders huchakatwa kwa kutumia mifumo ya kiotomatiki ya kiwango cha juu.
Je, instant execution ni nini?
Instant execution ni wakati brokers hutekeleza order yako kwa bei kamili unayoomba au haitekelezwi kamwe. Iwapo bei ya soko itabadilika wakati wa kuweka order, broker atatoa requote na kukuruhusu kukubali bei mpya au kughairi order hiyo. Iwapo unakabiliwa na requotes za mara kwa mara, unaweza kubadilisha mpangilio wa mkengeuko na kuruhusu mfumo kukubali bei ndani ya safu yako iliyoamuliwa awali inayokubalika kiotomatiki.
Je, market execution ni nini?
Market execution ni wakati orders zinatekelezwa papo hapo kwa bei ya sasa ya soko, ambayo inaweza kutofautiana na bei unayoona kutokana na mabadiliko ya mara kwa mara ya bei. Execution ya aina hii huhakikisha biashara ya haraka na ufikiaji wa soko wa mara moja.
Je, mchakato na sera ya order execution katika Exness ni ipi?
Katika Exness, order execution inahusisha njia za instant na market execution ambazo zimeundwa kulingana na mikakati tofauti ya biashara na mapendeleo ya hatari. Sera hii huhakikisha spreads thabiti wakati wa vipindi tete, execution ya haraka yenye slippage ndogo na kukataliwa na kanuni wazi za slippage kwa ajili ya execution ya haki. Miundo hii ya execution huwapa traders liquidity ya kina na athari ndogo ya soko.
Je, order ya trade hutekelezwaje katika Exness?
Katika Exness, mchakato wa execution ya order ya trade hutumia instant na market execution, ili kuhakikisha kuingia kwa haraka na kwa kutegemewa kwenye soko mara tu unapoweka' mipangilio ya akaunti yako na uko tayari kutrade.
Baada ya kusajili na kuthibitisha akaunti yako na kuweka pesa kwa mara yako ya kwanza, unaweza kuchagua jukwaa lako la biashara na kuongeza instruments unazopendelea. Iwe unatumia Terminali ya Exness au programu ya Exness Trade, unatekeleza trade kwa kuchagua kununua au kuuza instrument. Kisha trade hiyo huchakatwa kwa kutumia njia ya instant au market execution na kutekeleza orders zako kwa bei uliyoomba au bei bora zaidi inayopatikana ya soko.
Kila aina ya akaunti huja na mipangilio maalum ya execution kulingana na aina ya akaunti ya kutrade uliyochagua. Akaunti zote za Standard - Standard Cent, Standard - huja na market execution. Akaunti za Kitaaluma kama vile Raw Spread na Zero pia hutumia market execution. Akaunti ya Pro huja na instant execution kwa instruments zote za biashara na market execution kwa instruments zote za crypto na baadhi ya sarafu.
Je, kasi ya utekelezaji wa orders katika Exness ni?
Kwa market execution, Exness hutekeleza orders kwa bei bora zaidi inayopatikana sokoni kwa wakati huo kwa kasi ya execution inayokaribia ya papo hapo, hata wakati wa volatility ya juu. Kwa instant execution, Exness hutoa kiwango kilichopunguzwa cha requote, kwa hivyo trades hutekelezwa kwa ukatizwaji mdogo.
Je, orders hufungwa vipi katika instant execution?
Orders za instant execution hufungwa kwa njia sawa na zinavyofunguliwa; mara moja kwa bei ya sasa ya soko mara tu broker anapopokea order, bora tu bei iko ndani ya safu maalum au kiwango cha uvumilivu kilichowekwa na trader. Ikiwa bei itabadilika sana au iko nje ya kiwango kinachokubalika, order hiyo inaweza kunukuliwa na/au kukataliwa kulingana na mkengeuko uliowekwa.
Furahia order execution bila hitilafu
Gundua ufanisi wa kweli wa biashara na broker mkuu zaidi wa reja reja duniani.