Kufungua uwezo wa Fibonacci retracements katika biashara ya indices

Stanislav Bernukhov

Mtaalamu Mkuu wa Kutrade wa Exness

Anza kutrade

Huu sio ushauri wa uwekezaji. Utendaji wa awali sio dalili ya matokeo yajayo. Mtaji wako uko hatarini, tafadhali fanya biashara kwa uangalifu.

Shiriki

Ikiwa umekuwa ukitaka kuboresha biashara yako ya indices ukitumia zana mpya, basi indicator ya Fibonacci retracement inaweza kukufaa.

Kufanya biashara ya indices za stocks hubadilika-badilika. Kama trader, unaweza kuendelea kutafuta njia za kuboresha biashara yako na kufanya maamuzi bora ya kibiashara. Zana moja muhimu unayoweza kutumia ni Fibonacci retracement. Zana hii iliyopewa jina la mwanahisabati maarufu wa Kiitaliano Leonardo wa Pisa, au Fibonacci, imepata umaarufu katika ulimwengu wa biashara kutokana na uwezo wake wa kuvutia wa kutambua support na resistance levels zinazoweza kutokea.

Katika makala haya, tutaangazia kwa kina dhana ya Fibonacci retracements na kuchunguza jinsi unavyoweza kuzitumia kwa ufanisi kufanya biashara ya indices za stocks.

Kuelewa Fibonacci retracements

Fibonacci retracements ni zana za uchanganuzi wa kiufundi unazoweza kutumia ili kutambua viwango ambavyo trend ya bei inaweza kubadilika. Fibo retracements hupatikana katika mlolongo wa Fibonacci, mfululizo wa nambari za Fibonacci ambapo kila nambari ni jumla ya nambari mbili zilizoitangulia (0, 1, 1, 2, 3, 5, 8, 13, 21, na kadhalika). Katika biashara, uwiano wa Fibonacci unaoweza kutumia ni:

- 0.236 (23.6%)

- 0.382 (38.2%)

- 0.500 (50%)

- 0.618 (61.8%)

- 0.786 (78.6%)

- 1,000 (100%)

Ili kutumia zana hii, unahitaji kutambua hatua muhimu ya bei (ya juu au chini) na kisha kuchora mistari iliyolala katika uwiano huu muhimu wa Fibonacci. Mistari hii ya Fibonacci retracement hufanya kazi kama viwango vinavyowezekana vya support au resistance ambapo mabadiliko ya bei yanaweza kutokea.

Mfano wa kuunda wavu wa Fibonacci retracement. Chanzo: Tradingview.com

Hatua 5 za kutumia Fibonacci retracements kwa indices za stock

Sasa, hebu tujadili jinsi ya kutumia zana ya Fibonacci retracement wakati wa kufanya biashara ya indices kwa kutumia hatua 5 zilizo hapa chini.

Hatua ya kwanza. Tambua hatua kubwa ya bei

Hatua ya kwanza ya kutumia zana ya Fibonacci retracement ni kutambua hatua kubwa ya bei kwenye chati ya index ya stock. Hatua hii inaweza kuwa ya kupanda kwa bei au kushuka kwa bei ya hivi majuzi, kulingana na mkakati wako wa biashara. Kadri trend inavyoonekana kwa urahisi zaidi, ndivyo ilivyo bora zaidi.

Katika chati hii tunaweza kutambua kwa uwazi trend ya kupanda kwa index ya NASDAQ (USTEC). Chanzo: Tradingview.com

Hatua ya pili. Chora viwango vya Fibonacci retracement

Baada ya kutambua mabadiliko makubwa ya bei, tumia programu yako ya kuchora chati kuchora viwango vya Fibonacci retracement. Chora mstari uliolala kutoka sehemu ya chini zaidi ya mwenendo (mwisho wa mwenendo wa kushuka kwa bei) hadi sehemu ya juu kabisa ya mwenendo (mwisho wa mwenendo wa kupanda kwa bei) kwa trend ya kupanda au kinyume chake kwa trend ya kushuka. Hii huunda gridi ya Fibonacci retracement kwenye chati yako.

Mfano: Gridi ya Fibonacci retracement kwa index ya NASDAQ. Chanzo: Tradingview.com

Hatua ya tatu. Fafanua viwango vya Fibonacci retracement

Viwango vya Fibonacci retracement (23.6%, 38.2%, 50%, 61.8%, 78.6%, na 100%) huwakilisha viwango vinavyowezekana vya support na resistance. Hivi ndivyo unavyoweza kuvifafanua:

- 23.6% na 38.2%: hizi ni retracements ndogo. Katika trend ya kupanda, unaweza kupata fursa za kununua karibu na viwango hivi vya Fibonacci. Katika trend ya kushuka, zingatia fursa zinazowezekana za kuuza.

- 50%: kiwango hiki cha Fibonacci retracement mara nyingi huchukuliwa kuwa mojawapo ya viwango muhimu vya kurejea kwa bei kwa muda mfupi. Zingatia miitikio ya bei, kwa kuwa inaweza kuashiria mabadiliko yanayoweza kutokea au kuendelea kwa trends za soko.

- 61.8% na 78.6%: hivi ni viwango vikubwa vya Fibonacci retracement. Tafuta ishara dhabiti za kupanda au kushuka kwa bei karibu na points hizi, kwa kuwa zinaweza kupendekeza mabadiliko yanayoweza kutokea.

- 100%: kurejea kwa bei kwa muda mfupi kwa kiwango cha 100% kunamaanisha kubadilika kabisa kwa mwenendo wa awali. Kiwango hiki hakifikiwi kila mara, lakini kinapofikiwa, kinaweza kuashiria mabadiliko makubwa ya trend.

Hatua ya 4. Unganisha na zana zingine za uchanagnuzi wa kiufundi

Fibonacci retracements huwa na ufanisi zaidi zinapounganishwa na zana na indicators zingine za uchanganuzi wa kiufundi. Kwa mfano, unaweza kuzitumia pamoja na moving averages, mistari ya trend na oscillators ili kukusaidia kupata points zinazowezekana za kuingia na kutoka.

Hapa chini kuna mfano wa muunganisho wa moving average ya siku 50 na Fibonacci retracement ya 0.382 kwa index ya DE30 (index ya stock ya Ujerumani). Muunganisho (au kuunganishwa) wa zana hizi huthibitisha fursa ya uuzaji.

Mfano huu unaonyesha moving average ya siku 50 pamoja na Fibonacci retracement ya 0.382 kwa index ya DE30. Chanzo: Tradingview.com

Hatua ya 5. Unganisha na mifumo ya vinara

Unaweza kutumia mifumo ya vinara kama uthibitisho wa kiwango cha Fibonacci, kwa kuwa huonyesha mabadiliko ya muda mfupi ya hisia na inaweza kuonyesha sehemu bora ya biashara.

Huu hapa ni mfano kutoka index ya AUS200 mnamo Oktoba 2020. Baada ya kipindi cha kupanda kwa bei, bei ya index ilibadilika kuelekea kiwango cha Fibonacci retracement cha 0.618. Kufuatia mabadiliko haya, muundo wa engulfing ulionekana. Hii inaweza kutumika kama uthibitisho wa mabadiliko ya bei, kumaanisha kuwa bei inaweza kubadilisha mwelekeo.

Hii hapa ni picha ya muunganisho wa kiwango cha Fibonacci retracement cha 0.618 na muundo wa engulfing wa kinara uliotajwa hapo juu. Chanzo: Tradingview.com

Kutumia Fibonacci, hali ya 1: Trend ya kupanda katika S&P 500

Tuchukulie kuwa unachanganua S&P 500, na uone trend ya kupanda kutoka kwa point ya 4,338 hadi 4,470. Utumie viwango vya Fibonacci retracement kutoka kwa mwisho wa mwenendo wa kushuka kwa bei (4438) hadi mwisho wa mwenendo wa kupanda kwa bei (4470). Index inapoanza kurejea kwa bei kwa muda mfupi kwa kasi, huwa inapata uimarishaji juu kidogo ya kiwango cha 0.786. Unaweza kufikiria kuweka order ya limit order ya ununuzi katika kiwango hiki, kwa kuwa uwezekano wa kurejea katika kiwango hiki uko juu. Kurejea tena kimsingi ni kurejea kwa kiwango, ambacho, mara nyingi, huruhusu trader kuingia tena kwenye position kwa bei nzuri zaidi.

Bei hurejea tena kwenye kiwango hiki kwa kasi na kisha kurudi.

Katika mfano hapo juu, tunaona Fibonacci retracement ya index ya S&P 500 na bei kurejea kwenye kiwango cha 0.786. Chanzo: Tradingview.com

Kutumia Fibonacci, hali ya pili: trend ya kushuka kwa bei katika index ya HK50

Katika hali hii, unachanganua index ya Hang Seng (HK50), na utambue trend ya kushuka kutoka kiwango cha 20343 hadi 19302.

Uchore viwango vya Fibonacci retracement kutoka kwa mwisho wa mwenendo wa kushuka (20343) hadi mwisho wa mwenendo wa kupanda kwa bei (19302), na uone kwamba index inafikia resistance karibu na kiwango cha 50% cha kurejea kwa bei kwa muda mfupi (karibu na 19800). Hii inaweza kuwa point ya kuingia kwa trade ya uuzaji. Ili kupunguza hatari, unaweza kuweka order ya stop loss juu kidogo ya kiwango cha bei kurejea kwa muda mfupi cha 61.8% (karibu 19960).

Hapa kuna mfano wa kuweka trade ya uuzaji kwa index ya HK50 kwa kutumia Fibonacci retracement ya 50%. Chanzo: Tradingview.com

Faida na hasara za biashara ya Fibonacci

Hebu tuchunguze baadhi ya faida na hasara za kutumia indicator ya Fibonacci wakati wa kufanya biashara: kutoka kwa kuwa na uwezo wa kubashiri sehemu zijazo za support au resistance, na kutambua kurejea kwa bei kwa muda mfupi na kuendelea kwa mwenendo kwa changamoto zinazoweza kutokea za ubashiri usio sahihi, kuchanganyikiwa katika kuweka viwango, na kushawishi imani ya uongo.

Faida za Fibonacci

  • Indicators zinazotokana na Fibonacci hutumika kama indicators za kiwango cha juu, kumaanisha kuwa zinaweza kukusaidia katika kubashiri viwango vya support au resistance vya siku zijazo. Kinyume chake, viwango vya kawaida vya support and resistance kwa kawaida hutegemea hatua ya kihistoria ya bei. Ukibashiri kiwango kwa usahihi, bei huonekana kuitikia kwa kasi na kwa ukali, na kutoa uwezekano mkubwa wa uwiano wa faida/hasara.
  • Unaweza kutumia zana za Fibonacci kutambua kurejea kwa bei kwa muda mfupi na kuendelea kwa mwenendo wa bei. Matumizi haya yanaweza kukupa lengo linalowezekana la bei kwa position inayoleta faida.
  • Viwango tofauti vya Fibonacci vinaweza kuimarishana. Kwa mfano, ikiwa viwango kadhaa vya kurejea kwa bei kwa muda mfupi vinakusanyika karibu na bei mahususi, be hii huwa ya kuaminika zaidi.

Hasara za Fibonacci

  • Zana za ubashiri kama vile Fibonacci haziwezi kutoa viwango mahususi vya bei kila wakati. Ni bora katika kuonyesha sehemu zinazowezakana za mabadiliko ya bei. Utahitaji zana za ziada, kama vile mifumo ya vinara, ili kuthibitisha sehemu hizi.
  • Kuweka mipangilio ya viwango vya Fibo kwa usahihi wakati mwingine kunaweza kuwa na ugumu. Kunaweza kuwa na viwango vingi vya chini na vya juu, na usipokuwa mwangalifu, unaweza kuchagua viwango visivyo sahihi unapounda wavu wako wa Fibo. Kutumia zana za Fibonacci ipasavyo huhitaji mazoezi fulani.
  • Kuwa mwangalifu unapotumia viwango vya Fibonacci kwani vinaweza kukupa hisia zisizo za kweli za kujiamini au usalama. Kwa kuwa hakuna mbinu zinazohakikisha mafanikio ambazo zitabashiri kila mara viwango vya juu na vya chini kwa mafanikio wakati wa kufanya biashara katika masoko ya kifedha, zana hii ya uchanganuzi wa kiufundi inapaswa kutumiwa kwa busara.

Maswali yanayoulizwa sana

Ni vigumu kusema Fibonacci retracement nzuri ni ipi. Katika soko ambalo bei inapanda, kurejea kwa bei kwa muda mfupi huonekna kuwa kati ya 23.6% na 50%, kwa kuwa kubadilika kwa mwenendo wa bei kwa kawaida hukuwa chini. Katika soko ambalo bei yake inashuka, matokeo yanaweza kuwa makubwa kutokana na kuongezeka kwa volatility na yanaweza kuzidi 70%. Hata hivyo, kurejea kwa bei kwa muda mfupi kwa 50% labda ndio maarufu zaidi. Baadhi ya indicators, kama vile indicator ya Ichimoku, huundwa karibu na tukio la 50% la Fibonacci retracement.

Unaweza kutumia Fibo retracements kwenye timeframe yeyote kwa sababu masoko ya kifedha mara nyingi hujirudia. Hata hivyo, kuitumia kwa muda mfupi hufanya iwe vigumu kutambua kwa usahihi wavu wa Fibonacci retracement kutokana na ‘kubadilika-badilika kwa soko’ kwa ziada. Kwa hivyo, inapendekezwa kuwa utumie zana hizi kwa timeframes refu zaidi ya chati ya dakika 5.

Dhana ya kurejea kwa bei kwa muda mfupi hufanya kazi tu ikiwa trend bado inaendelea. Kama trader, dhana yako kuu ni kwamba trend itaendelea. Hata hivyo, ikiwa trend tayari imepita, kujaribu kungojea kubadilika kwa bei kwa muda mfupi kunaweza kuwa hatari. Zaidi ya hayo, ikiwa hatua ya bei inasababishwa na habari, inaweza kusababisha mabadiliko makubwa katika hisia za soko na uwezekano wa kubadilika. Katika hali kama hizi, kutumia Fibo retracements pia kunaweza kuwa na hatari kwako.

Kuna kuendelea kwa mwenendo wa Fibonacci kadhaa, lakini maarufu zaidi ni 1.236% na 1.618%. Wakati mwingine, wakati soko linakwenda haraka, inaweza kufikia kiwango cha 2.618%. Hata hivyo, inashauriwa kupima volatity ya soko katika hali halisi. Ikiwa lengo lililotarajiwa liko ndani ya safu ya volatility ya kila siku au ya kila wiki, uwezekano wa kufikia lengo hili huongezeka kwa kiasi kikubwa. Unaweza kutumia zana kama vile indicator ya average true range (ATR) ili kukokotoa volatility.

Wavu wa Fibonacci ni mfululizo wa viwango, vilivyoundwa kiotomatiki wakati trader anaunganisha nukta mbili (juu na chini) kwenye chati. Wavu wa Fibonacci huelekeza trader kwenye kiwango cha bei kinachowezekana cha kurejea kwa bei kwa muda mfupi na kuendelea kwa mwenendo. Zana za Fibonacci pia zinajumuisha safu za Fibo, saa za maeneo za Fibo, chaneli za Fibo na miduara ya Fibo.

Hapa kuna mfano wa zana ya ‘Fibonacci wedge’, kama inavyotumika kwa XAUUSD. Chanzo: Tradingview.com

Tumia Fibonacci retracements kwa mkakati wako wa biashara ya indices

Fibonacci inaweza kuwa zana muhimu kwako unapofanya biashara ya indices. Inaweza kukusaidia kutambua viwango vinavyowezekana vya support na resistance, na kuamua wakati wa kuingia au kuondoka kwenye trade. Hata hivyo, ni muhimu kukumbuka kuwa hakuna zana ya uchanganuzi wa kiufundi ambayo inahakikisha mafanikio na kwamba udhibiti wa hatari ni muhimu katika biashara ya indices za stock.

Ili kutumia Fibonacci retracements kwa ufanisi, sharti uzijumuishe na zana zingine za uchanganuzi wa kiufundi na uendelee kuboresha ujuzi wako wa uchanganuzi wa kiufundi kupitia mazoezi na majaribio.

Kwa kufanya hivyo, unaweza kufungua uwezo wa Fibonacci na kuongeza nafasi zako za mafanikio katika soko la indices.

Je, uko tayari kuboresha biashara yako? Anza kufanya biashara ya indices katika Exness leo. Tafuta akaunti sahihi kwa mahitaji yako.

Shiriki


Anza kutrade

Huu sio ushauri wa uwekezaji. Utendaji wa awali sio dalili ya matokeo yajayo. Mtaji wako uko hatarini, tafadhali fanya biashara kwa uangalifu.