Kuelewa spreads katika forex - Mtazamo wa kina wa ada za brokers

Michael Stark

Kiongozi wa Maudhui ya Kifedha wa Exness

Anza kutrade

Huu sio ushauri wa uwekezaji. Utendaji wa awali sio dalili ya matokeo yajayo. Mtaji wako uko hatarini, tafadhali fanya biashara kwa uangalifu.

Shiriki

Ikiwa unashangaa spread katika forex ni nini basi hauko peke yako. Pengine ni mojawapo ya maswali ya kwanza ambayo trader yeyote huuliza anapovutiwa na biashara ya mikataba ya utofauti. Spreads ni ada ambazo unalipa kwa broker wako ili uweze kununua na kuuza. Hivi ndivyo brokers wengi hupata pesa. Ukubwa wa spread unaweza kuathiri mapato yako kwa kiasi kikubwa. Ili uweze kuweka mipango mapema, uthabiti wa spread ni muhimu.

Makala haya yanajibu swali ‘Spread katika forex ni nini?’ kwa urahisi na kwa undani. Yanaelezea athari zinazowezekana za spread kwa mapato ya traders na yanaangazia aina mbalimbali za spreads zinazopatikana. Pata maelezo ya options zinazopatikana kwenye aina mbalimbali za akaunti na jinsi zinavyofanya kazi kwa ajili yako, kulingana na mkakati wako na mbinu yako ya kufanya biashara.

Je, spread ni nini?

Spread ni tofauti ya bei kati ya bei ya ununuzi na ya uuzaji ya instrument. Ni ada ambayo broker kama Exness hutoza kwa kutoa huduma zake kwa wale ambao wangependa kutrade forex. Kimsingi, spreads ni gharama muhimu zinazotozwa ili kulipia gharama za broker wako kama vile mishahara ya wafanyakazi, kudumisha seva na majukwaa, na kuleta huduma mpya.

Jinsi spreads hufanya kazi

Spreads hufanya kazi kwa kugawanya bei ya soko ya instrument katika bei mbili katika jukwaa la biashara. Bei hizi mbili zinaitwa ‘ask’ na ‘bid’. Unanunua kkatika bei ya ask - ambayo hukuwa juu kila wakati - na unafunga trades zako za ununuzi kwa bei ya bid. Unapouza, kinyume chake ni kweli. Unafungua kwa bei ya bid na unafunga kwa bei ya ask. Hii ndiyo sababu huwa unaona hasara ndogo mara tu unapofungua trade kila wakati.

Unapotumia jukwaa la tovuti la Exness, unaweza kuona bei hizo mbili kwenye chati na kwenye upande wa kulia wa skrini. Hasara ndogo inayoonekana mara baada ya trade kufunguliwa ndiyo spread.

Spreads za exness, tofauti kati ya bei mbili, kwa kawaida huanzia takriban 0.005% hadi 0.01% ya thamani ya kawaida ya contract. Hii inaweza kubadilika kulingana na instrument unayofanyia biashara, habari na wakati wa siku. Ikiwa wewe ni trader unayezingatia biashara ya muda mfupi, unaweza kulenga kutrade instruments kwa spreads za chini kabisa.

Unapoweza kupata spreads

Njia ya kuaminika zaidi ya kupata spread ya sasa ya bid-ask ya instrument ni kuangalia chati yake kwenye jukwaa la MT5 au Exness. Unaweza kupata spreads kwenye chati mahususi ya instrument na katika Taarifa za Soko kwenye MT5 au menyu ya ‘kuongeza’ kwenye jukwaa la tovuti la Exness'.

Unaweza kufungua chati mpya na kuona spread ya instrument hiyo kwenye menyu ya kuongeza.

Unaweza pia kupata spreads za wastani kwenye tovuti ya Exness chini ya taarifa kuhusu instruments. Ukurasa huu hukuonyesha spread ya wastani ya hivi majuzi kwa jozi kuu za sarafu.

Je, spread ya forex ni nini na ni kiasi gani? Ukurasa huu kwenye tovuti ya Exness hukuonyesha wastani wa spreads wa siku iliyotangulia.

Kumbuka kuwa spreads zilizonukuliwa kwenye tovuti si sawa na spreads za moja kwa moja unazoona kwenye jukwaa la biashara. Spreads kwenye tovuti ni wastani wa siku iliyotangulia, wakati soko lilikuwa limefunguliwa.

Kwa nini spreads ni muhimu

Kukuwa na spread ya chini au iliyobana ni muhimu kwa sababu inamaanisha kuwa unaweza kuokoa pesa. Ukilipa gharama za chini kutrade, jumla ya mapato yako itakuwa juu au jumla ya hasara yako chini.

Vile vile, ni muhimu kuwa na spread ‘thabiti’ kwa sababu hiyo hurahisisha kupanga mapema. Ikiwa una ufahamu wa kuaminika wa spread unayohitaji kulipa, unaweza kujaribu, na kuwa na uhakika zaidi kwamba matokeo hayo ni sahihi.

Ikiwa wewe ni mgeni katika biashara, ni muhimu pia kuwa na spreads thabiti katika vipindi ambapo habari fulani zinaweza kuathiri soko. Kwa kuzingatia volatility ya soko la forex na shughuli katika masoko kuhusu habari muhimu zaidi kama vile ripoti ya ajira ya Marekani (pia inajulikana kama ripoti ya mashirika yasiyo ya kilimo au 'NFP' kwa ufupi), haiwezekani kuwa na fixed spread ya kweli katika nyakati kama hizo. Lakini baadhi ya brokers au market makers kama Exness wanaongoza katika kudumisha uthabiti.

Je, aina za spread ni gani?

Spreads, tofauti kati ya bei ya bid na ask, hufanya kazi kwa njia kadhaa. Kwa kawaida, traders na brokers huweka kategoria za spreads kulingana na zinabadilika kwa kiasi gani na, kwa kiasi kidogo, zinabadilika baada ya muda upi. Mabadiliko kama haya ya spreads yanaweza kusababishwa na baadhi ya sababu tofauti, lakini liquidity na habari kuu ndio muhimu zaidi.

Floating spreads

Sehemu kubwa ya spreads hukuwa ‘floating’, pia inajulikana kama ‘spreads zinazobadilika’. Huwa zinabadilika, kulingana na mambo mbalimbali kama vile wakati wa siku, masharti ya soko, habari, liquidity, na orodha ya wakati halisi ya ununuzi na uuzaji kwa instrument fulani. Floating spreads zinaweza kutofautiana sana kanzia chini ya pip moja - katika vipindi visivyo na shughuli nyingi wakati instrument imefunguliwa kwa muda - hadi pips 12 au zaidi, wakati wa habari kuu au vipindi vya kiwango cha juu kama vile muda wa kufunguliwa na kufungwa. Kuna aina mbili zaidi kuu za spread katika biashara ya forex.

Fixed spreads

Fixed spread ni spread ambayo hukuwa sawa kila wakati na haibadilika. Ni nadra sana kupata fixed spreads katika biashara ya rejareja, kwa sababu haziwakilishi soko 'halisi'. Katika soko lolote la kifedha, sharti spreads zibadilike hata kama ni kidogo, kulingana na orodha ya wakati halisi ya ununuzi na uuzaji kwa instrument fulani kwa broker mahususi. Wakati wa mizunguko muhimu ya habari kwa mfano, bei hubadilika haraka sana kwa sababu ya kiwango cha juu, hali ambayo inaweza kusababisha pending orders kutekelezwa moja baada ya nyingine. Katika nyakati kama hizo, brokers wanahitaji kutoa spread ya juu, ili kupunguza hatari kwao na kwako, mteja.

Tofauti thabiti ya bei ya ununuzi na uuzaji

Spreads thabiti zinakaribiana na fixed spreads kuliko floating spreads, lakini bado zinatofautiana na zote mbili. Katika Exness, spreads thabiti kubaki sawa kwa takriban 95% ya muda, na kwa kawaida huwa hazibadiliki zaidi ya 50% kutoka kwa spread ya wastani kwa muda uliosalia.

Tofauti na floating spreads —ambazo zinaweza kuwa juu kwa mara kumi au mamia kuliko wastani karibu na habari kuu au kufunguliwa na kufungwa kwa soko — spreads thabiti ni tofauti. spreads thabiti zinaweza kurahisisha biashara yako. Sio tu kwamba zinaweza kukuokolea pesa kwa wastani, lakini pia zinaweza kukusaidia kupanga trades zako vizuri na kwa ujasiri zaidi.

Jinsi ya kukokotoa spread

Sasa kwa kuwa unaelewa jibu la msingi la ‘Spread katika biashara ni nini?’ sharti ujifunze jinsi spread hukokotolewa kabla ya kuanza kutrade. Sio lazima ujue kila kitu au kufanya ukokotoaji wote katika kichwa chako. Kikokotoo cha uwekezaji cha Exness kinaweza kukokotoa spread na kukusaidia kubaini gharama za spreads kati ya mambo mengine mengi.

Pips na points

Pips kimsingi ni kipimo cha kiasi ambacho bei ya sarafu inasonga, lakini pia hutumiwa kupima spreads. Mara nyingi katika forex, pip ni sehemu ya nne ya desimali ya quotation:

GBPUSD UNUNUZI 1.27841 UUZAJI 1.27829

Hapa pip ni nambari ya pili ya mwisho ya bei zilizonukuliwa. Spread, basi, ni pips 1.2.

Unapaswa kukumbuka kuwa nafasi ya pip hutofautiana kulingana na instrument inayofanyiwa trade. Kwa mfano, metali na cryptocurrencies hufanya kazi tofauti na jozi nyingi za forex. Jozi zilizo na yen pia ni tofauti. Njia rahisi zaidi ya kujifahamisha na pips na jinsi zinavyofanya kazi ni kwa kutumia muunganisho wa akaunti ya demo na Kikokotoo cha uwekezaji cha Exness.

Points hutumiwa kwa kawaida katika MetaTrader 4 na MetaTrader 5. Point ni sehemu moja kati ya kumi ya pip. Ikiwa MT4 itakuonyesha kuwa spread ya dola-yen ni points 8, hii inamaananisha kuwa spread ni pips 0.8. Ni muhimu kukumbuka tofauti kati ya pips na points kwa sababu vipengele vingi kwenye jukwaa hilo kama vile stop losses, take profits na trailing stops zinaweza kosa ufanisi mkubwa unapovichanganya.

Thamani ya pip/‘pip profit’

Faida au hasara kutokana na mwenendo wa pip moja ina majina mbalimbali, ikiwa ni pamoja na thamani ya pip, pip value, pip profit na mengine. Yote haya yanarejelea thamani ya mienendo ya bei kwa pip moja.

Unahitaji vitu vitatu ili kukokotoa thamani ya pip: contract size (kwa kawaida 100,000 ya sarafu ya msingi ya forex), kiasi ambacho unafanyia trade katika lots, na ukubwa wa pip. Hebu tuseme unafanya trade ya cable (GBPUSD) ukitumia lot ndogo (lot 0.01). Hivi ndivyo ukokotoaji ungekuwa:

0.1 x $100,000 x 0.0001 = $1

Hiyo ndiyo thamani ya pip. Ili kukokotoa gharama ya spread, unazidisha thamani hiyo kwa ukubwa wa spread kama ilivyoelezwa hapo juu. Matokeo katika mfano huu yatakuwa spread ya $1.20.

Kumbuka, hauitaji kufanya ukokotoaji huu wewe mwenyewe isipokuwa ikiwa unafurahia hesabu na ungependa kujaribu maarifa yako. Mfumo wowote unaotumia unakufanyia, na unaweza pia kutumia Kikokotoo cha uwekezaji cha Exness ili kupata thamani ya spread yoyote.

Options zako za spreads na njia mbadala, ada

Je, spread katika biashara ni nini? Spreads ni njia ya 'chaguo-msingi' ya kulipa ili kutrade kwa traders wengi. Hata hivyo, brokers wengi, ikiwa ni pamoja na Exness, hukupa wepesi wa kuchagua jinsi ungependa kulipia huduma wanayokupa.

Ikiwa unapendelea scalping au kutumia baadhi ya aina za algoriti za muda mfupi, huenda usipate bei rahisi ya spread. Ndiyo maana Exness alianzisha akaunti za Zero na Raw Spread ili kukupa options zaidi.

Akaunti za spread

Baadhi ya akaunti zinazopatikana katika Exness huwa na spreads kama kielelezo cha bei. Baadhi zimeainishwa kama akaunti za standard na zingine ni akaunti za kitaaluma.

Akaunti za Standard na Pro hutofautiana hasa katika execution. Akaunti ya Standard hutumia market execution pekee, ilhali akaunti ya Pro hutumia instant execution hapo kwa karibu instruments zote, isipokuwa kwa cryptocurrencies.

Akaunti ya Pro pia hutoa spreads za chini zaidi zinazopatikana katika Exness bila kutozwa ada.

Kwa traders wengi, akaunti ya Pro hutoa gharama za chini zaidi za kutrade. Spreads kwa akaunti za Pro kwa wastani ziko juu kuliko akaunti za Zero, lakini hakuna ada. Iwapo ungependa kutumia mkakati wowote unaozingatia wakati, isipokuwa scalping na trade ya siku moja, na uko tayari kuweka kiasi cha pesa cha chini zaidi cha $200, akaunti ya Pro inaweza kukufaa. Hata hivyo, ikiwa hungependa kuweka kiasi hicho, bado unaweza kutrade kwenye akaunti ya Standard.

Akaunti za zero

Exness pia hutoa option ya akaunti ya Zero, mojawapo ya akaunti zake za kitaaluma ambazo hazitozi ada. Kwa akaunti ya Zero kwa ujumla, instruments mbalimbali hazitozwi spreads.

Ikiwa wewe ni scalper au trader wa algoriti, akaunti ya Zero inaweza kuwa chaguo nzuri. Unaweza kupanga trades za muda mfupi na za mienendo ya juu ukitumia akaunti hii, ambayo inaweza kuwa na ufanisi zaidi kwa sababu ada hazibadiliki kwa instruments zote. Mabadiliko yoyote kwa ada hutangazwa mapema.

Tafadhali kumbuka kuwa akaunti za Zero hazina spreads za sufuri kwa kila instrument kila wakati. Exness hutoa spreads thabiti za sufuri kwa instruments 30 bora. Kwa hakika, baadhi ya jozi nadra sana kama vile Dola ya Australia-Krone ya Denmaki (AUDDKK) na hisa za watu binafsi zinazofanyiwa trade kwa kiwango cha chini kama vile Broadcom (AVGO) zitatozwa spread fulani karibu kila wakati pamoja na ada.

Akaunti za Raw Spread

Ikiwa ungependa kutumia mikakati mbalimbali ya kutrade, akaunti ya Raw Spread inaweza kukufaa. Akaunti hii ya kitaaluma hufanya kazi kwa muunganisho wa spreads na ada.

Je, spread ni nini kwa biashara ya jozi ya sarafu kwa kutumia ya akaunti ya Raw Spread hasa? Spreads hapa hukuwa juu kuliko akaunti ya Zero lakini hukuwa chini kuliko kwa Akaunti ya Standard au Pro. Ada hukuwa juu kuliko akaunti ya Standard au Pro (ambayo haitozi ada) lakini hukuwa chini kuliko akaunti ya Zero.

Faida kuu inayoweza kupatikana kwa kutumia akaunti ya Raw Spread ni kwamba inakupa uwezo wa kurekebisha mkakati wako kulingana na hali katika masoko ya kifedha. Ikiwa mkakati wako wa kawaida au trade ya algoriti haifanyi kazi, kwa mfano, unaweza kuhama kwa muda hadi kwenye biashara ya siku moja, biashara ya muda mfupi au biashara ya positions - kisha urejee kwenye algoriti yako baadaye, bila kuhitaji kubadili akaunti ili kupunguza gharama.

Je, Exness ingependa kupata pesa kutokana na hasara za wateja?

Hapana. Takriban 90% ya faida ya Exness hutokana na spreads. Nyingine hutoka kwa ada za akaunti ya Zero na Raw Spread. Kiasi kidogo pia hutoka kwa swaps, ambazo ni ada za usiku kucha zinazotozwa kwa baadhi ya instruments.

Kwa Exness tunathamini uwazi na ni msingi wa mafanikio yetu. Tunaamini kuwa kufanya kazi kwa kuzingatia maslahi ya wateja wetu pia ni kwa manufaa yetu kama shirika.

Hii ndiyo sababu tulikuwa mojawapo wa brokers wa kwanza kuchapisha data yetu ya kifedha iliyokaguliwa. Unaweza kuangalia ukaguzi wa kifedha wa Exness kwenye tovuti yetu, ili kuona pesa ambazo wateja wetu kwa pamoja hutoa kwa wastani kila robo mwaka. Hatutaki upoteze pesa katika biashara kwa sababu tunapata pesa kutokana na spreads.

Maswali yanayoulizwa sana

Spreads ni gharama za kutrade ambazo hupunguza mapato yako na kuongeza hasara zako. Kwa kawaida ungependa kuepuka spreads za juu kwa sababu huwa zinafanya iwe ngumu kwako kupata faida ya kutosha. Kila wakati unapofungua trade, ikiwa spreads zinahusishwa, utaona hasara ndogo iliyosababishwa na spread.

Ikiwa wewe ni scalper, huenda utapendelea kutumia akaunti inayotozwa ada badala ya inayotozwa spread ili kuokoa pesa kwa muda mrefu. Unaweza pia kuchagua akaunti ya Raw Spread, ambayo husawazisha spreads na ada.

Kwa wastani, spreads za Exness huanzia takriban 0.1% hadi 0.005% ya jumla ya thamani yenye leverage ya kila trade. Hii inamaanisha kuwa spreads kwa kawaida huwa na athari ndogo kwa faida yako, isipokuwa katika hali nadra.

Spread ya 0.3 inamaanisha spread ya pips 0.3 au points 3. Kwa mfano, euro-dola yenye spread ya 0.3 inaweza kunukuliwa kama 1.07376/1.07373 katika MT5. Ili kutrade lot ya kawaida ya $100,000 katika hali hiyo kungegharimu $3 katika spread.

Mara nyingi, spreads hunukuliwa katika pips, sio points. Hata hivyo, ukiona spread inayonukuliwa katika MT4 au MT5 kama 3, hiyo inamaanisha points 3, kwa maneno mengine pips 0.3. Kuna points 10 katika pip, kwa hivyo spread ya pip 1 na spread ya points 10 ni sawa. Hata hivyo, wakati wa kuangalia spread ya jozi ya sarafu, unahitaji kujua ikiwa spread inayonukuliwa ni kwa points au pips ili kujua ukubwa wake.

Kutambua spread nzuri kwa forex kunakutegemea wewe, kama trader, na masharti ya soko. Traders wengi wanaweza kuzingatia spread nzuri kuwa iliyo chini kiasi, — karibu na pips mbili au chini yake kwa jozi kuu za forex - na thabiti karibu kila wakati.

Kuwa na spreads thabiti hurahisisha kupanga mapema na kutathmini matokeo yako, na kuleta kiwango cha kubashirika kwa trades zako.

Kikwazo cha kawaida cha spreads zinazobadilika sana ni kwamba kwa kawaida huwa chini wakati watu wachache wangependa kufanya biashara, lakini huwa juu sana karibu na ripoti za habari, na kufunguliwa na kufungwa kwa soko. Ingawa ni jambo lisiloepukika kwamba spreads kwa wakati mwingine zitaongezeka karibu na habari muhimu zaidi, spreads zako katika Exness ni thabiti zaidi kuliko wastani.

Je, kwa nini uamini Exness kutoa spread thabiti katika forex?

Huhitaji kutuamini kuwa tutatoa spread thabiti, na hupaswi tu kukubali tunachosema. Badala yake, angalia wewe mwenyewe. Kwa kuwa sasa unajua kuhusu spread ya forex, sajili akaunti ya Standard ya moja kwa moja —hakuna haja ya kuweka pesa —kisha ufungue jukwaa lako unalopendelea na uangalie spreads za moja kwa moja kila wakati.

Iwapo ungependa kutathmini spreads za Exness kwa akaunti za Pro, Zero na Raw Spread, unaweza kufungua akaunti ya demo kwa kila akaunti na kuelewa mienendo huko bila kuhitaji kuweka funds. Unapopata akaunti inayokufaa na uko tayari kufanya trade, unaweza kuchagua kufungua akaunti ya moja kwa moja ya kufanya biashara kwa kutumia pesa halisi.

Pata maelezo zaidi kuhusu spreads za Exness, mafao ya kipekee na vipengele vya kukusaidia kuboresha matumizi yako ya biashara. Jaribu spreads thabiti za Exness kwa akaunti ya demo ya Standard leo.

Shiriki


Anza kutrade

Huu sio ushauri wa uwekezaji. Utendaji wa awali sio dalili ya matokeo yajayo. Mtaji wako uko hatarini, tafadhali fanya biashara kwa uangalifu.